If Only
If Only ni filamu ya mahaba iliyotolewa 2004 iliyoongozwa na Gil Junger na kuigizwa na Jennifer Love Hewitt pamoja na Paul Nicholls.
If Only | |
---|---|
Imeongozwa na | Gil Junger |
Imetayarishwa na | Jill Gilbert Jeffrey Graup Jennifer Love Hewitt |
Nyota | Jennfer Love Hewitt, Paul Nicholls, Tom Wilkinson Lucy Davenport |
Muziki na | Adrian Johnston |
Imehaririwa na | William M. Anderson Padriac McKinley |
Imesambazwa na | Sony Pictures Home Entertainment |
Imetolewa tar. | 23 Januari 2004 |
Ina muda wa dk. | Dakika 92 |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Hadithi
haririIan Wyndham (Paul Nicholls) ni mwanabiashara Muingereza anayeishi na mpendwa wake Samantha Andrews (Jennifer Love Hewitt) jijini London. Ian hamtii maanani Sam na humchukulia kimzahamzaha na hii inafmfanya Sam kuwa mnyonge kwani anampenda Ian kwa dhati. Nusu ya kwanza ya filamu hii inatunaonyeshwa siku moja ambapo Sam anapandwa na hasira baada ya kuteta na Ian. Baada ya kukorofishana, Sam anapanda teksi na kupata ajali na kuaga dunia. Kwa huzuni, Sam anaenda nyumbani na kulala kitandani akiwa mpweke. Anapoamka asubuhi, anampata Sam kando ya kitanda - kumaanisha kuwa yote yaliyopitika yalikuwa ni ndoto tu. Baada ya hapo, Ian anagundua kuwa hakuwa akimchukulia Sam kwa dhati; na Ian anapata nafasi nyingine ya kurekebisha makosa aliyoyafanya. ian anafanya juhudi zake zote kumpenda Sam kwa dhati na mwishowe, yeye ndiye anayekufa kwa ajali badala ya mpenzi wake. Kifo kinampata anapomshika mkono kwa mara ya mwisho.
Utayarishaji
haririFilamu hii ilirekodiwa mnamo Novemba 2002 hadi Januari 2003. Filamu hii ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye studio ya Saratosa Film Festival mnamo Januari 2004.Ilionyeshwa nchini Marekani mnamo 15 Januari 2006 kwenye stesheni ya ABC na nchini Uingereza mnamo 28 Julai 2009 kwenye stesheni ya Hallmark.
Wimbo
haririJennifer Love Hewitt aliandika nyimbo zote mbili za "Love Will Show You Everything" na "Take My Heart Back"
Viungo vya nje
hariri- If Only | American romantic drama movie (Official Site) Ilihifadhiwa 2 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine.
- If Only katika Internet Movie Database