Imilchil au Imilshil (Kiarabu: إملشيل‎) ni mji mdogo katika jimbo la Midelt nchini Morocco, katika milima ya atlas yenye idadi ya watu takribani 1,858. Inapatikana usawa wa mita 2119 katika bonde la Asif Mellulen. Eneo la Imilchil ni makazi ya kabila la Ayt Hdiddu. Vivutio vya utalii katika eneo hili ni mapango ya Axyam (Akhyam), maporomoko ya maji ya Ziz Gorges na bonde la igherman.

Ramani ya Moroko
Ramani ya Moroko
Mji wa Imlchil, Moroko
Mji wa Imlchil, Moroko

Sherehe ya Ndoa

hariri

Mji wa Imilchil ni kiashirio cha utamaduni wa watu wa Berber, inayofahimika kwa sherehe zake, iliyotambulika rasmi kama sherehe za Betrothal - Souk Aam au Agdoud N'Oulmghenni. Hadithi inahusu watu wawili wa makabila tofauti waliopendana ila familia zao hazikuwaruhusu kuonana. Majonzi yaliwapelekea kulia mpaka vifo vyao, na kutengeneza maziwa ya jirani ya Isli na Tislit karibu na Imilchil. Familia zilifikia uamuzi wa kuanzisha siku ya kumbukizi ya vifo vya wapenzi hao pale watu wa makabila yao wakioana ndipo sherehe ya ndoa ya Imilchil ilipozaliwa.[1]

Marejeo

hariri
  1. "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-02. Iliwekwa mnamo 2009-05-31.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Imilchil kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.