Immigrant Song
"Immigrant Song" ni wimbo wa bendi ya Kiingereza ya "Led Zeppelin" ya muziki wa rock . Imetengenezwa kwa kuwekewa sauti ya mwimbaji Robert Plant.[1] Wimbo huu ulijumuishwa kwenye albamu yao ya 1970, Led Zeppelin III na kutolewa kama singo. Rekodi kadhaa za moja kwa moja pia zimetolewa kwenye albamu mbalimbali za Led Zeppelin. Wasanii wengine wamerekodi matoleo ya wimbo huo au pia kuutumbuiza katika majukwaa ya muziki.
Japokuwa kundi hili la Led Zeppelin linaonekana ni kundi la kutoa muziki katika mfumo albamu,singo hii ya "Immigrant Song" ni miongoni mwa singo zilizofanya vizuri na kupendwa sana.[2] Umaarufu wa wimbo huu umesababisha kujumuishwa katika albamu kama vile Led Zeppelin Remasters (1990) na Early Days: The Best of Led Zeppelin, Vol. 1 (1999).[2][3]
Historia yake
hariri"Immigrant Song" uliandikwa wakati wa ziara ya Led Zeppelin huko Iceland, Bath na Ujerumani katika majira ya joto ya 1970. Tarehe ya ufunguzi wa ziara hii ilifanyika huko Reykjavík, Iceland, ambayo ilipelekea Plant kuandika maneno ya wimbo huu. Alifafanua katika mahojiano:
Hatukuwa wabishi ... Tulitoka nchi ya barafu na theluji. Tulikuwa wageni wa Serikali ya Iceland kwenye misheni ya kitamaduni zaidi. Tulialikwa kucheza tamasha huko Reykjavik na siku moja kabla ya sisi kuwasili watumishi wote wa umma waligoma na tamasha lilikuwa lighairishwe. Chuo kikuu kilituandalia ukumbi wa tamasha na lilikuwa tamasha ya ajabu na la aina yake. Jibu kutoka kwa watoto lilikuwa la kushangaza na tulikuwa na wakati mzuri. Wimbo wa 'Immigrant Song' ulihusu safari hiyo na ulikuwa wimbo wa ufunguzi wa albamu hiyo ambao ulikusudiwa kuwa tofauti sana.[4]
Siku sita baada ya kuonekana kwa Led Zeppelin huko Reykjavik, bendi iliimba wimbo huo kwa mara ya kwanza katika tamasha la huko Bath.[5]
- ↑ Curtis, James M. (1987). Rock Eras: Interpretations of Music and Society, 1954–1984. Popular Press. uk. 292. ISBN 978-0-87972-369-9.
- ↑ 2.0 2.1 Erlewine, Stephen Thomas. "Led Zeppelin – Early Days: The Best of Led Zeppelin, Vol. 1". AllMusic. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Erlewine, Stephen Thomas. "Led Zeppelin – Led Zeppelin Remasters". AllMusic. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Welch, Chris (1994). Led Zeppelin. London: Orion Books. uk. 55. ISBN 1-85797-930-3.
- ↑ Lewis, Dave; Pallett, Simon (1997). Led Zeppelin: The Concert File. London: Omnibus Press. ku. 50–51. ISBN 0-7119-5307-4.