Indinaviri (Indinavir (IDV)), inayouzwa kwa jina la chapa Crixivan, ni dawa inayotumika kutibu HIV/UKIMWI pamoja na dawa nyingine[1], lakini sio matibabu ya mstari wa kwanza.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, na mawe kwenye figo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya ini, kisukari na ugawaji tena wa mafuta mwilini.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Ni kizuizi cha protease.[1]

Indinaviri ilipewa hati miliki mwaka wa 1991 na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 1996.[3][1][4] Nchini Marekani, inagharimu takriban Dola 450 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Indinavir Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Indinavir (Crixivan) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 509. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-20. Iliwekwa mnamo 2021-08-05.
  4. "Crixivan". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Indinavir Sulfate Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)