Injera ni aina ya chapati ambayo ni chakula cha asili ya Ethiopia, Eritrea na Somalia. Unga wa matefi (mtefi ni nafaka ya pekee katika nyanda za juu za Ethiopia) huchanganywa na maji na kisha kuachwa hadi unapochacha baada ya siku chache. Baada ya hapo uji huo unakuwa tayari kupikia chapati. Injera huliwa na saladi au mchuzi uitwao Wat. Mchuzi huu huweza kuwa wa nyama ya ng'ombe au mbuzi. Kwakuwa unga wa Injera huwa umechacha, ladha yake huwa na uchachu.

Chakula cha Kiethiopia cha injera na aina za wat

Nje ya nyanda za juu watu wanatumia unga wa mchele, mahindi au nafaka nyingine ingawa kiasili ni matefi.

Viungo vya Nje

hariri