Jérémy Doku
Jérémy Baffour Doku (amezaliwa 27 Mei 2002) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kimataifa kutoka Ubelgiji[1], anaecheza soka la kulipwa katika ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza akiwa anacheza kama winga ndani ya klabu ya Manchester City[2]. Anajulikana sana kwa uwezo wake mkubwa wa kukimbia akiwa na mpira pamoja na kudribo mpira. Anafikiriwa kuwa ndio mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu mwenye umri mdogo kwa sasa katika nafasi yake.
Doku alianza safari yake ya soka la kulipwa akiwa na klabu yake ya Anderlecht ya nchini Ubelgiji msimu wa 2018-19, akiwa ameifungia magoli 5 katika michezo 34 aliyo cheza katika misimu yote akiwa na klabu hiyo. mwaka 2020 alijiunga na klabu ya Rennes FC[3] inayo cheza ligi kuu ya Ufaransa iitwayo Ligue 1 ambako aliifungia magoli 10 katika michezo 75 aliyo cheza kabla ya kujiunga na mabingwa wa Uingereza msimu wa 2021/22 mwezi August 2023 kwa ada ya uhamisho ya €65 million.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jérémy Doku kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |