Jamal Abdelmaji Eisa Mohammed

Jamal Abdelmaji Eisa Mohammed (alizaliwa 25 Agosti 1993) ni mwanariadha kutoka Sudani anayeshindana kimataifa kwenye mbio ya mita 5,000 na 10,000.[1] Mohammed alikuwa ni miongoni mwa wanariadha 29 kutoka kwenye taaluma 12,ambao walishiriki kuliwakilisha shirika la Timu ya Olimpiki ya Wakimbizi katika Tokyo Olimpiki ya 2020 .

Jamal Abdelmaji Eisa Mohammed, 2022

Mwaka 2003, alipokuwa na umri wa miaka 10, wafuasi wa Janjaweed walikichoma kijiji chao na kuwauwa watu 97, akiwemo baba yake.Mnamo mwaka 2010 alikimbia machafuko ya nchini Sudani ya kivita mjini Darfur akiwa na umri wa miaka 17,na alitumia siku tatu kuvuka jangwa la Sinai kutoka misri kuelekea Israeli kwa miguu ambapo ndipo alipopatiwa msaada kama mkimbizi. Alipata ajira mjini Tel-Aviv na kujiunga na klabu ya riadha ya The Alley Runners mnamo 2014. Alimaliza nafasi ya 40 kwenye Mabingwa wa vilabu Ulaya 2017, wa 30 mnamo 2018 na wa 22 mwaka 2019 kwenye usaili wa tarehe 3 Februari Albufeira, ureno.

Marejeo

hariri
  1. "Jamal Abdelmaji EISA MOHAMMED | Profile". worldathletics.org.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jamal Abdelmaji Eisa Mohammed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.