Jamhuri F.C.
Jamhuri Sports Club, ni klabu ya mpira wa miguu yenye makao kisiwani Pemba, Zanzibar.
Jamhuri ilianzishwa mwaka wa 1953, na wakati huo iliitwa klabu ya Barghash.[1] Baada ya mapinduzi ya Zanizibar mwaka 1964, jina lilibadilishwa na kuwa Jamhuri.
Timu pinzani kuu ni Mwenge S.C. kwani timu zote zinapatikana Wete. Jamhuri ilikuwa timu ya kwanza kutoka kisiwani Pemba kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar.
Marejeo
hariri- ↑ "Zanzibar - List of Cup Winners". www.rsssf.org. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.