Jengo la Wesley W. Posvar
Chuo Kikuu cha Pittsburgh kina jengo la masomo linaloitwa Jengo la Wesley W. Posvar au Posvar, lakini awali lilijulikana kama Forbes Quadrangle.[1] Jengo[2] la Wesley W. Posvar ni jengo muhimu sana katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh na lina mchango mkubwa. Ndani ya jengo hili, kuna ofisi nyingi, ikiwa ni pamoja na Shule ya Elimu, Chuo cha Masomo ya Jumla (College of General Studies), Shule ya Umahiri ya Mambo ya Umma na Kimataifa (Graduate School of Public and International Studies), na Shule ya Sanaa na Sayansi (inayojulikana kama Shule ya Dietrich).
Jengo la Wesley Wentz Posvar
haririKatika Chuo Kikuu cha Pittsburgh, kulikuwa na mtu mashuhuri aliyeitwa Wesley Wentz Posvar, ambaye alikuwa Rais wa Chuo wa kumi na tano. Alizaliwa Septemba 14, 1925, huko Topeka, Jimbo la Kansas, nchini Marekani. Mwaka wa 1946, alijiunga na jeshi. Baadaye, alisomea katika Chuo Kikuu cha Oxford na Chuo Kikuu cha Harvard. Baada ya kuondoka jeshini, alihamia Chuo Kikuu cha Pittsburgh ambapo alikuwa Rais wa Chuo. Wesley Wentz Posvar amejulikana sana kwa mchango wake katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh, ambapo aliongoza ujenzi wa shule nyingi. Aliaga dunia Julai 27, 2001.
Ujenzi
haririJengo la Wesley W. Posvar lilijengwa na Louis Valentour. Jengo hili lina ukubwa wa 69,184.4 m². Jengo la Posvar liko karibu na Jengo la David Lawrence Hall, Jengo la Sheria la Barco, na Maghorofa ya Litchfield. Jengo hili lina jumla ya madirisha 2,000, ofisi 574, vyumba 30 vya mikutano, na kumbi 3 za mihadhara. Jengo la Posvar liligharimu karibu dola milioni 38,000,000, au shilingi bilioni 5. Kuna lifti zinazowahudumia walimu na wanafunzi. Pia kuna kituo cha Jengo la Posvar kinachojulikana kama Nyumba ya Sanaa (Galleria). Hapa, kuna michoro mbalimbali. Mojawapo ya michoro hiyo ni mchoro unaojulikana kama "Kutaalamika na Kufurahi" (Englightment and Joy), ambao ulichorwa na Virgil Cantini.[3]
Masomo ya Kimataifa na Masomo ya Kiafrika katika Jengo la Posvar
haririChuo Kikuu cha Pittsburgh kina masomo ya kimataifa ambapo wanafunzi wanaweza kusoma kuhusu nchi na mataoifa mbalimbali. Pia, wanaweza kujifunza lugha mbalimbali kama Kifaransa, Kiitaliano, na Kijapani. Kuna walimu wanaotokea nchi za Kiafrika ambao wanafundisha lugha kama Kiswahili, Kiamhara, Kiyoruba, Kiwolof, Kiakani, na Kiarabu.[4] Wanafunzi wengi huchagua kusoma masomo ya Kiafrika. Hapa, wanaweza kupata vyeti au shahada katika masomo ya Kiafrika. Kuna ofisi maalum kwa masomo ya Kiafrika ambapo wanafunzi wanaweza kupata ushauri kutoka kwa mshauri wa wanafunzi anayeitwa Anna-Maria Karnes. Chuo Kikuu cha Pittsburgh hutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma lugha za Kiafrika kama Kiswahili na Kiarabu kupitia tuzo kama vile FLAS (Foreign Language and Area Studies).
- ↑ "Request Rejected". historicpittsburgh.org. Iliwekwa mnamo 2024-04-29.
- ↑ "Wesley W. Posvar Hall | Campus Tour". www.tour.pitt.edu. Iliwekwa mnamo 2024-04-29.
- ↑ "Wesley W. Posvar Hall--1st Floor, Galleria". Pittsburgh City Paper (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-29.
- ↑ "Welcome to the Center for African Studies | African Studies Program". www.ucis.pitt.edu. Iliwekwa mnamo 2024-04-29.