Jeremy Lee Renner (amezaliwa tar. 7 Januari 1971) ni mwigizaji wa filamu na vilevile mwanamuziki kutoka nchini Marekani. Renner ameonekana kwenye filamu katika kipindi cha miaka ya 2000, hasa katika nyusika za usaidizi, kama vile kwenye Dahmer (2002), S.W.A.T. (2003), Neo Ned (2005), na 28 Weeks Later (2007).

Jeremy Renner

Renner kwenye sherehe ya 2014 San Diego Comic-Con International
Amezaliwa Jeremy Lee Renner
7 Januari 1971 (1971-01-07) (umri 53)
Modesto, California, U.S.
Kazi yake Mwigizaji/mwanamuziki
Miaka ya kazi 1995–hadi sasa

Hatimaye akaja kuwa maarufu na ufahamiko wa haja kwa kucheza nyusika kadhaa katika filamu ya The Hurt Locker (2009), The Bourne Legacy, na The Avengers (2012). Alizapata kuchaguliwa kama Mwigizaji Bora katika Tuzo za Academy Award kwa uhusika wake wa mwaka wa 2009 kwenye filamu iliyoshinda tuzo hizo The Hurt Locker. Mwaka uliofuata kaonekana kwenye mafilamu makubwakubwa kama vile The Town.

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jeremy Renner kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.