" Jerusalema " ni wimbo wa DJ wa Afrika Kusini na mtayarishaji wa rekodi Master KG akimshirikisha msanii wa Afrika Kusini Nomcebo . Wimbo ulitolewa tarehe 29 Novemba 2019 baada ya kupata mapokezi mazuri toka kwa mashabiki mtandaoni, na kisha video iliyofuata tarehe 21 Desemba. Baadaye ilijumuishwa kwenye albamu ya pili ya Master KG yenye jina sawa, iliyotolewa mnamo Januari 2020. [1] Hatimaye iliyotolewa katika huduma ya kutazama mubashara mtandaoni Julai 10 mwaka 2020, [2] baada ya hapo ikazidi kupata umaarufu zaidi katikati ya mwaka 2020, imezidi kupata umaarufu kimataifa kutokana na mashindano ya #JerusalemaChallenge. Marudio ya wimbo iliyomshirikisha mwimbaji wa Nigeria Burna Boy ilitolewa mnamo 19 Juni 2020, na kuupeleka wimbo kwenye chati za Billboard za Amerika. Tangu wakati huo imefikia nambari moja nchini Ubelgiji na Uswizi, huku ikishika nafasi katika kumi bora ya nchi zingine nyingi za Uropa. Remix ya pili iliyo na mwimbaji wa Venezuela Micro TDH na mwimbaji wa Colombia Greeicy ilitolewa mnamo 17 Septemba 2020. [3]

"Jerusalema"
Wimbo wa Master KG featuring Nomcebo

kutoka katika albamu ya Jerusalema

Umetolewa 29 Novemba 2019 (2019-11-29)
Umerekodiwa 2019
Mtunzi * Kgaogelo Moagi
  • Nomcebo Zikode
Mtayarishaji Master KG


Athari

hariri

Wafuasi wa Spotify KG waliongezeka hadi kufikia zaidi ya milioni 1.2 kufuatia umaarufu kuongezeka kwa wimbo huo. [4]

Mashindano ya Kucheza

hariri

Mashindano ya kucheza yalifuatia baada ya kikundi cha densi cha marafiki huko Angola wanaofanya densi katika video ya wazi, [5] ilisaidia wimbo huo kuenea mtandaoni. [6] #JerusalemChallenge, ambayo imelinganishwa na Macarena, [7] ilizalisha video za densi kutoka nchi nyingi, pamoja na Italia, Uhispania, Ufaransa, Jamaica na Canada. [4] [8]

Marejeo

hariri
  1. "Jerusalema by Master KG on Apple Music". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-24. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Jerusalema (feat. Nomcebo Zikode) [Edit] - Single by Master KG on Apple Music". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-24. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Jerusalema (feat. Micro TDH & Greeicy & Nomcebo Zikode) [Remix] - Single de Master KG". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-03. Iliwekwa mnamo 23 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Master KG's 'Jerusalema' reaches over 50m views on YouTube". IOL. 26 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "It reminds me of the 'Macarena' - Master KG on 'Jerusalema' going global". Times Live. 20 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "SA artist's 'Jerusalema' song takes world by storm". CapeTownEtc. 21 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Jolly, Tamlyn (25 Julai 2020). "WATCH: Empangeni takes on Jerusalema dance challenge". Zululand Observer. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Ngcobo, Nokuthula (26 Julai 2020). "WATCH: Nuns and priests dance to 'Jerusalema' by Master KG". ECR. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri