Jim Doyle
James Edward Doyle, Jr. (amezaliwa 23 Novemba 1945) ni mwanasheria na mwanasiasa wa Marekani ambaye aliweza kutumikia kama gavana wa arobaini na nne wa Wisconsin, akitumikia kuanzia januari 6 mwaka 2006 hadi kufikia januari 3 ya mwaka 2011. Katika uchaguzi wake wa kwanza wa kuwania ugavana wa Wasconsin aliweza kumshinda gavana Scott McCallum aliyekuwa madarakani kwa kuwa na wingi wa asilimia 45 kwa asilimia 41, Mgombea wa chama cha Libertarian Ed Thompson alishinda asilimia 10 ya kura. Japokuwa mnamo mwaka 2002 wanademokrasia waliongeza namba za magavana, Doyle alikuwa ni mmoja wa kipekee baina yao kuondoa kiti cha republican. Doyle aliweza pia kutumikia kama mwanasheria mkuu wa Wisconsin kwa takribani miaka 12 kabla hajaweza kuwa gavana. Kwa sasa ni wakili wa mawakili katika ofisi ya Madison, Wisconsin inayomilikiwa na Foley & Lardner na pia anatumikia katika bodi ya ushirika ya Epic systems. [1][2]
Marejeo
hariri- ↑ "Andrews, Mark Björnsen, (born 12 July 1952), Partner (formerly Deputy Chairman), SNR Denton UK LLP (formerly Denton Wilde Sapte), solicitors, 2000–11; Consultant, Dentons UKMEA LLP (formerly SNR Denton UK), 2011–13", Who's Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2022-08-10
- ↑ "Employers Win Supreme Court Approval of Waivers". Management Report for Nonunion Organizations. 41 (8): 1–2. 2018-07-13. doi:10.1002/mare.30414. ISSN 0745-4880.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jim Doyle kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |