Jim Sinclair

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Jim Sinclair ni mtetezi na mwandishi kutoka Marekani mwenye usonji ambaye alisaidia kuanzisha harakati ya neurodiversity. Sinclair, pamoja na Xenia Grant na Donna Williams, walianzisha Autism Network International (ANI). Sinclair alikua mratibu wa awali wa ANI. Sinclair ni mtetezi wa msimamo wa kupinga tiba ya usonji, akieleza kuwa usonji ni sehemu muhimu ya utambulisho wa mtu na haipaswi kutibiwa. Sinclair ni intersex na hutumia viwakilishi vya kijinsia Xe/Xem/Xyr. [1]

Marejeo

hariri
  1. Silberman, Steve (2015). NeuroTribes: The Legacy of Autism and the Future of Neurodiversity. Avery An Imprint of Penguin Random House. ku. 432–434. ISBN 978-0-399-18561-8.
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jim Sinclair kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.