John Brooks (mwamuzi)
John Brooks ni mwamuzi wa Ligi Kuu ya kandanda Uingereza, ambaye alipandishwa cheo mnamo Juni 2021. Kabla ya hapo, Brooks alikuwa mwamuzi mteule wa Kundi la 2 la waamuzi tokea mwaka 2018, na kabla ya hapo, alikuwa mwamuzi msaidizi.[1]
Mnamo Desemba 2021, Brooks alichezesha mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu kati ya Wolves na Burnley huko Molineux.[2]
Mnamo Februari 11 2023, Brooks kwa makosa aliondoa bao la Brighton & Hove Albion Pervis Estupiñán dhidi ya Crystal Palace. Mtaalamu aliyepewa jukumu la kuchora mistari alishindwa kuchora mstari hadi kwa mlinzi wa mwisho wa Crystal Palace na kumtambua kimakosa James Tomkins kama mchezaji wa Crystal Palace aliye karibu zaidi na lango lake na kwa wakati alikuwa ni mchezaji mwenzake Marc Guéhi.[3][4]Baada ya picha kuwasilishwa kwa Brooks, alihukumu vibaya hali hiyo na bila kukusudia akafutilia mbali bao la Brighton & Hove.
Mkutano wa dharura uliitishwa na PGMOL na mkuu wao Howard Webb baada ya tukio hilo. Kufuatia mkutano huo, John Brooks alipumzishwa na hivyo kutokuchezesha mechi zake mbili zilizofuatia.[5]
Marejeo
hariri- ↑ "Four new referees for 2021/22 Premier League".
- ↑ "New Premier League ref John Brooks takes charge at Brighton".
- ↑ "VAR technician was partly to blame for John Brooks error during Crystal Palace vs Brighton - The Athletic". 2023-02-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-27. Iliwekwa mnamo 2023-02-27.
{{cite web}}
: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link) - ↑ "Decision made as VAR official punished after Brighton blunder at Crystal Palace", SussexWorld. (en-GB)
- ↑ MacInnes, Paul. "Referee John Brooks taken off VAR duty for two matches after Brighton error", The Guardian, 2023-02-13. (en-GB)