John Hocking amezaliwa tarehe 6 Agosti 1957 nchini Australia. Ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa, Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Yugoslavia ya zamani (ICTY),)[1] na wakati huohuo, Msajili wa Mifumo ya kuendesha Mahakama za Kimataifa za mauaji ya Kimbari (UNMICT).[2]

John Hocking


Assistant-Secretary-General of the United Nations (ASG)

Registrar of the International Criminal Tribunal for the former Yugoslavia

Registrar of the Mechanism for International Criminal Tribunals


Wasifu hariri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alimteua John Hocking kwa awamu mbili, kwanza tarehe 15 Mei 2009 na tena tarehe 15 Mei 2013, kuongoza Usajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Yugoslavia ya zamani,[3] chombo muhimu cha Mahakama hiyo ambacho kinatoa msaada wa kisheria, kidiplomasia na utawala kwa Waamuzi, upande wa Mashtaka, na Ulinzi.[4] Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alimteua Hocking tarehe 18 Januari 2012 kama Msajili wa kwanza wa Mifumo ya kuendesha Mahakama za Kimataifa za Mauaji ya Kimbari[5] na pia aliaminika kwa kukabidhiwa dhamana ya kuanzisha kazi za Mahakama hiyo.[6]

Hocking alijiunga na ICTY mnamo mwaka 1997 kama afisa mratibu wa sheria katika kesi ya kwanza kujumuisha mashauri yenye mashitaka zaidi ya moja kwenye Mahakama ya kimataifa mauaji ya kimbari ya Yugoslavia ya zamani (ICTY), kesi ya Celebici.[7] Pia aliwahi kuwa Afisa Mkuu wa Sheria katika Kitengo cha Rufaa cha Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Yugoslavia ya zamani (ICTY) na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).[8] Alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya ICTY mnamo mwaka 2004 hadi 2009.[9] Kabla ya ushiriki wake na Umoja wa Mataifa, Hocking ameshika nyadhifa mbalimbali kama mshauri wa kisheria na sera ya Kimataifa nje na ndani ya nchi, ikiwa ni pamoja na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) mjini Paris, alifanya kazi katika kituo cha redio na televisheni katika nchi ya Australia (Special Broadcasting Service), Chuo cha Filamu mjini London na pia Tume ya Filamu ya Australia.

Katika miaka ya awali baada ya kumaliza masomo yake na kama njia ya kuendeleza taaluma yake, Hocking aliwahi kuwa msaidizi wa kisheria wa Jaji Michael Kirby,[10] aliyekuwa raisi wa Mahakama ya Rufaa na Mwamuzi wa Mahakama kuu ya Australia na Mwanasheria wa haki za binadamu Geoffrey Robertson Q.C[11] jijini London.

Hocking alipata wadhifa wa kuwa Wakili kupitia taasisi ya Lincoln’s Inn mjini London,[12] kwa mahakama kuu ya Victoria na New South Wales mjini Australia. Pia ana Shahada ya Sheria na sifa kutoka London School of Economics, Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Sydney,[13] na Shahada ya Sayansi kutoka Chuo kikuu cha Monash mjini Melbourne, Australia. Alihudhuria pia mafunzo ya Uongozi wa juu katika shule ya Serikali ya Havard Kennedy.[14]

Marejeo hariri