John Momose Cheyo ni Mbunge katika Bunge la Tanzania.

John Cheyo ni mojawapo wa viongozi wakongwe wa vyama vya upinzani Tanzania. Cheyo alipata umaarufu sana nchini Tanzania katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa 1995 ambapo alisema kwa ufupi kwamba sera zake ni "kuwajaza watanzania mapesa". Hii ilikuwa ni sera inayokaribishwa sana kwa sababu wakati huo maisha yamekuwa ni magumu sana kwa watanzania wengi na nchi zingine za dunia ya tatu. Shida kubwa ni kwamba alishindwa kujieleza kuwa hayo mapesa angeyatoa wapi ilihali nchi inamadeni kama ilivyo nchi nyingi za dunia ya tatu

Chanzo hariri