Josip Bozanić

Kadinali wa Kroatia na Askofu Mkuu wa Zagreb

Josip Bozanić (alizaliwa Rijeka, Yugoslavia, sasa Kroatia, 20 Machi 1949) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Kroatia ambaye alikuwa Askofu Mkuu wa Zagreb kuanzia 1997 hadi 2023. Awali alikuwa Askofu wa Krk kuanzia 1989 hadi 1997. Aliteuliwa kuwa kardinali mwaka 2003.

Josip Bozanić

Wasifu

hariri

Josip Bozanić alizaliwa akiwa mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Ivan Bozanić na Dinka Valković. Alisoma katika seminari ndogo ya Pazin na Kitivo cha Theolojia cha Rijeka na Zagreb, ambako alipata Shahada ya Uzamili katika theolojia. Alipadrishwa tarehe 29 Juni 1975 na Askofu Karmelo Zazinović, ambaye alimtumikia kama katibu binafsi hadi 1976.[1]

Marejeo

hariri
  1. Acta Apostolicae Sedis (PDF). Juz. la LXXXIX. 1997. uk. 596. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2023.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.