Joti
Lucas Lazaro Mhuvile (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Joti; amezaliwa 9 Julai 1982) ni mwigizaji wa filamu na michezo ya televisheni kutoka nchini Tanzania. Sanaa yake mara nyingi hufanya na Mpoki ambaye ni mwenzi wake tangu alipoanza shughuli za sanaa. Kwa pamoja wanaitwa "Mpoki na Joti". Wametengeneza mifululizo ya filamu za vichekesho kadha wa kadha. Ulio maarufu sana ni ule wa Kung Fu Bongo - ambao ndani yake wamecheza na Kingwendu.
Maisha ya awali
haririLucas Lazaro Mhuvile amezaliwa 9 Julai 1982 katika mkoa wa Morogoro Wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Biro. Lucas Lazaro Mhuvile maarufu Joti ni msanii wa vichekesho, mshereheshaji na mzalishaji wa vipindi ya televisheni na redio nchini Tanzania. Joti amekuwa katika sanaa kwa zaidi ya miaka 20 na ni moja ya wasanii mahiri zaidi wa vichekesho kuwahi kutokea nchini Tanzania.
Maisha yake ndani ya sanaa
haririLucas Lazaro Mhuvile alikuwa na kipaji cha kuchekesha tangu alipokuwa mtoto. Alikuwa mchekeshaji maarufu katika vikundi vya maigizo shuleni kwao. Kutokana na yeye kupenda sana kazi hii ya uchechi, baada ya kumaliza shule alijiunga na vikundi mbalimbali vya maigizo kwa ajili ya kujiendeleza na kujitafutia uzoefu zaidi. Joti alianza kujizolea umaarufu baada ya kujiunga na kikundi cha Nyota Ensemble ambacho kilikuwa kikionyesha ucheshi katika kituo cha ITV. Hata hivyo watu wengi hawakuvutiwa sana na jinsi walivyokuwa wanacheza ucheshi huo kwenye kituo cha ITV. Baadaye Joti na Mpoki waliamua kuungana na wasanii wenzake na kuanzisha kundi jipya la ucheshi lililojulikana kwa jina la The Comedy. Kundi hili lilirusha ucheshi wao kwenye kituo cha Televisheni cha EATV. Kundi hili lilikuja kwa kasi na kumuweka msanii Joti katika chati ya juu kabisa kutokana na umahili wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika vichekesho. Joti ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana nchini Tanzania kwani anauwezo wa kucheza kama mwanamke, mzee kikongwe n.k na kuuvaa uhusika huo na watu wakafurahi. Kutokana na umahili wake huo amekuwa na majina mengi tofauti ya kisanii kutokana kucheza nafasi nyingi katika kundi lake.
Vikundi alivyopitia
haririJoti alipitia vikundi kadhaa vya maigizo kabla ya kujiunga na kundi lake analofanya kazi sasa la Ze komedi. Mwaka 2000 - 2001 Joti alikuwa mwingizaji katika kundi la Nyepenyo, baadaye 2001 - 2003 lijiunga na kundi lingine la Sun rise na 2002 - 2003 alichezea kundi liitwalo Nyota Ensemble. Joti ali-maarufu kama Hami Jay, Da Kiboga, Mzee Simbawanga, Asha Ngedere na Andunje alianza kuhamishia usanii wake kwenye TV baada ya kukutana na rafiki yake kipenzi Mpoki. Joti aliingia mkataba na kituo cha Televisheni cha ITV na kuanza kucheza michezo ya kuchekesha iliyojulika kama Joti na Mpoki. Kikundi cha Joti anachochezea kwa sasa ni ZE COMEDI, kikundi hiki kinaundwa na wasanii watano ambao ni Joti, Masanja maarufu kama mkandamizaji, Mpoki, Maki Regani maarufu kama Shemeji,
Vituo vya Televisheni alivyopitia
haririVituo vya Televisheni alivyopitia kama mchekeshaji maarufu nchini Tanzania ni ITV, EATV na TBC1.
Viungo vya Nje
hariri- Mpoki na Joti kwenye CB Archived 27 Septemba 2010 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |