Juan Miguel Echevarría

Juan Miguel Echevarría Laflé (alizaliwa 11 Agosti 1998) ni mwanariadha kutoka nchini Kuba ameshiriki kwenye miruko mirefu[1]. Aliiwakilisha nchi yake kwenye michuano ya Dunia 2017, kukosa fainali. Baadae alikuja shinda medali ya dhahabu 2018 kwenye World Indoor Championships kwa alama ya mita 8.46 (27 ft 9 in).

Juan Miguel Echevarría mnamo mwaka 2017
Juan Miguel Echevarría mnamo mwaka 2017

Rekodi yake bora kwenye michuano ni mita 8.68 (28 ft 5+12 in) michezo ya nje ya Bad Langensalza mwaka 2018 kwenye upepo wa mita kwa sekunde +1.7 (3.8mph) na mita 8.46 (27 ft 9 in) mchezo wa ndani 2018 kule Birmingham. Aliruka mita 8.92(29 ft 3 in) kule Havana tarehe 10 Machi 2019, akisaidiwa na upepo wa kasi ya +3.3 mita kwa sekunde(7.4mph), mbali na rekodi ya taifa ya Kuba ya mita 8.71(28 ft 6+34 in). Wakati, mruko huu haukubaliki kwenye rekodi ya nchini Kuba sababu ikiwa usaidizi mkubwa utokanao na upepo, ila umetambuliwa kama mruko mrefu kwenye mashindano chini ya vigezo vyovyote kwa takriban miaka 24, na mruko wa tano mrefu kurukwa chini ya vigezo vyovyote kuwahi tokea[2]

Marejeo

hariri
  1. "Juan Miguel ECHEVARRÍA | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
  2. "Echevarria leaps wind-assisted 8.92m in Havana | REPORT | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.