K-rupt
Carlton Williams Bongo Juma (15 Novemba 1979 - 29 Novemba 2003) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka mjini Nairobi huko nchini Kenya. Alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama K-rupt. Alikuwa akifanyia shughuli zake katika studio ya Ogopa Deejays.[1]
K-rupt | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Carlton Williams Bongo Juma |
Pia anajulikana kama | K-rupt |
Amezaliwa | 1981 |
Asili yake | Nairobi, Kenya |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa |
Miaka ya kazi | 1999-2003 |
K-rupt aliuawa na jelaha la pigo moja la risasi akiwa katika basi dogo (matatu) akiwa anatokea Nanyuki akielekea Nakuru. K-rupt alipanda basi hilo kwa lengo la kwenda kufanya tamasha lake huko mjini Nakuru. Wanyang'anyi hao walipanda basi hilo na kutoa agizo kwa dereva asimamishe gari katika eneo la Karuga, kama kilomita saba hivi kutoka kando ya barabara. Mashuhuda walieleza ya kwamba K-rupt, aliyekomea umri wa miaka 24, alikuwa akibishana na majambazi hao ambao pia ndiyo waliomtandika risasi, na kumuua kwa riasi moja tu. Waliutupa mwili wake katika Msitu wa Laikipia kulingana na taarifa ya polisi.[2]
Diskografia
hariri- "Changamshwa"
- "Tukawake"
- "Chacha"
- "Dada Njoo"
- "Bamba" (E-Sir feat. Big Pin & K-rupt)
Marejeo
hariri- ↑ "Wasanii: Krupt - Brief Bio". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-20. Iliwekwa mnamo 2013-12-27.
- ↑ "Kenya rap star K-rupt shot dead". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-28. Iliwekwa mnamo 2013-12-27.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)