Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia
(Elekezwa kutoka KAST)
"Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia" (kifupi: KAST) ni kamusi iliyoandaliwa na wataalamu wa TUKI na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995.
Kamusi hii inakusanya maneno ya kisayansi na ya kiteknolojia kwa utaratibu ufuatao:
- neno la Kiswahili
- maana yake kwa Kiingereza katika mabano
- maelezo yake kwa Kiswahili
Mwishowe kuna faharasa ya Kiingereza inayoweza kutumiwa kama kamusi ndogo ya Kiingereza-Kiswahili ya maneno ya kisayansi.
Kati ya kamusi za Kiswahili hii ni hatua kubwa mbele katika ukuzaji wa Kiswahili hata ikionyesha bado mapengo na kasoro mbalimbali.
Hali halisi kiasi kikubwa cha maneno yaliyokusanywa humo hayatumiwi tena.
Marejeo
hariri- Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia (KAST). Dar es Salaam, Tanzania: Ben & Co. Ltd., 1995.