KEMRI
Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya au 'Kenya Medical Research Institute' (KEMRI) kwa Kiingereza ni shirika la serikali lililoanzishwa na Amri ya marekebisho ya Sayansi na Teknologia ya mwaka 1979, kama shirika la kitaifa la kufanya utafiti wa afya nchini Kenya. KEMRI imekua kutoka kwa mianzo yake nyenyekevu miaka 27 iliyopita hadi ikawa kiongozi wa kufanya utafiti wa afya ya binadamu. Taasisi hii ni mojawapo ya taasisi zinazoongoza katika ubora barani Afrika na dunia nzima. Ofisi za KEMRI ziko Mbagathi Road, Nairobi.
Maono
hariri"Kuwa kituo cha ubora katika ukuzaji wa afya bora".
Utume
hariri"Kuimarisha ubora wa afya na maisha ya binadamu kwa kutumia utafiti".
Wito
hariri"Utafiti wa afya bora".
Marejereo
hariri- Tovuti Rasmi ya KEMRI Ilihifadhiwa 24 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.