Kaliopi (Perge katika Pamfilia, leo nchini Uturuki, karne ya 3 - Pompeiopoli, Kilikia, leo nchini Uturuki, 300 hivi) alikuwa kijana Mkristo wa Perge ambaye aliuawa kutokana na imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano wa Dola la Roma[1].

Inasemekana alisulubiwa kichwa chini miguu juu.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 7 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.