Kaliua ni kata iliyo makao makuu ya Wilaya ya Kaliua katika Mkoa wa Tabora, Tanzania.

Kaliua
Kaliua is located in Tanzania
Kaliua
Kaliua

Mahali pa Kaliua katika Tanzania

Majiranukta: 5°3′32″S 31°47′36″E / 5.05889°S 31.79333°E / -5.05889; 31.79333
Nchi Tanzania
Mkoa Tabora
Wilaya Kaliua
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 16,270
Tovuti:  https://kaliuadc.go.tz/

Wilaya hiyo mpya ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012. Kaliua ipo njia panda ya reli iendayo Kigoma kwa upande wa magharibi na Mpanda kwa upande wa kusini. Kaskazini imepakana na wilaya ya Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.

Wilaya ya Kaliua ina uwanja wa ndege mdogo kwa shuguli ndogondogo za anga. Ina huduma za simu za mkononi, posta, shule za sekondari ikiwa ni pamoja na Kaliua High School.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 16,270 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,073 waishio humo.[2]

Kwa ujumla Kaliua ni mji unaokua kwa kasi katika ukanda wa magharibi.

Mazao yanayolimwa Kaliua ni tumbaku, karanga, mahindi, alizeti, ufuta. Ufugaji ni muhimu. Asali ni moja ya mazao yanayovunwa sana, pia uvuvi hufanyika katika maeneo oevu ya usinge, swampu n.k.

Kwenye mwaka 2013 mbunge wa wilaya hiyo alikuwa profesa Juma Athumani Kapuya, aliyewahi kuwa waziri wa elimu, kazi na maendeleo ya vijana, wizara ya ulinzi n.k.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Kaliua - Mkoa wa Tabora - Tanzania  

Ichemba | Igagala | Igombemkulu | Igwisi | Ilege | Kaliua | Kamsekwa | Kanoge | Kashishi | Kazaroho | Kona Nne | Makingi | Milambo | Mkindo | Mwongozo | Nhwande | Sasu | Seleli | Silambo | Ufukutwa | Ugunga | Ukumbi Siganga | Usenye | Ushokola | Usimba | Usinge | Uyowa | Zugimlole


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaliua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.