Kampuni ya Viatu ya Bacup ni kampuni ya kutengeneza viatu iliyo na makao yake katika kijiji cha Stacksteads,karibu na Bacup, Lancashire,Uingereza. Kampuni hii ilianzishwa katika mwaka wa 1928 na Ernst Goodwin. Kampuni ya Bacup ni mojawapo ya kampuni bora, zinazojulikana kwa kuunda viatu, zilizofunga viwanda vyake katika mwisho wa miaka ya 1990 na kuanza kuagiza viatu kutoka Mashariki ya Mbali. Wanaowasilisha viatu hivyo wana makao yao nchini Uchina (nchi ambayo kampuni hii imeanzisha makao yake mpya),Vietnam na Uhispania.[1]

Kampuni ya Viatu ya Bacup
Jina la kampuni Kampuni ya Viatu ya Bacup
Ilianzishwa 1928
Mwanzilishi Ernst Goodwin
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji
Makao Makuu ya kampuni Lancashire,Uingereza
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu
Nchi Uingeeza
Tovuti Tovuti rasmi ya Kampuni ya Bacup

Ukuaji wa Kampuni ya Viatu ya Bacup

hariri

Tangu mwaka wa 1928, kampuni hii imenawiri na ikawa wasambazaji wengi, wa viatu vyao, katika nchi ya Uingereza.Makao yao makuu yalipatikana Stacksteads.

Sekta kuu za kampuni hii ni viatu vya Wanaume, Wanawake, Watoto na vya kutumika katika mazoezi ya michezo. Wameajiri wauzaji wa rejareja wanaojulikana sana kwa mfano Tesco,ASDA ,Woolworths na Littlewoods wakiwa wateja wao wakuu.

Katika mwaka wa 2002,kampuni hii ilifungua sehemu mpya iliyoitwa Alpha Logistics & Warehousing ya kuhusisha matumizi kamili ya maghala yao yote na matumizi bora ya wafanyikazi wenye vipaji.

Pamoja na upanuzi wa makao makuu ya kampuni hii,Bacup wameanzisha aina mpya ya viatu vya wasichana.Aina hii inaitwa Redfoot After Party Shoe na ni bidhaa za kampuni hii zilizosajiliwa katika sheria.

Marejeo

hariri
  1. Wide Fitting Famous Footwear and Famous Foot Care Products by Ilihifadhiwa 14 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine. - Natureform.co.uk
  2. Lancashire County Council: Lancashire Profile Ilihifadhiwa 1 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
  3. Retailing Ilihifadhiwa 9 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. - UK News 1998
  4. SHOEINFONET Wanted - Employee Ilihifadhiwa 7 Julai 2007 kwenye Wayback Machine.
  5. Bacup Shoes Archived 2012-02-09 at Archive.today

Viungo vya nje

hariri
  1. [1]