Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania
Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania (kwa Kiromania Biserica Română Unită cu Roma, Greco-Catolică) ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.
Linafuata mapokeo ya Ukristo wa Ugiriki na kutumia liturujia ya Ugiriki likiongozwa na Askofu mkuu kabisa, kwa sasa kardinali Lucian Mureşan.
Mbali ya jimbo kuu la Fǎgǎraş na Alba Iulia, nchini Romania kuna majimbo manne: Oradea Mare, Cluj-Gherla, Lugoj na Maramureş.[2]
Kanisa hilo lina pia jimbo la Mt. George huko Canton, Marekani linalowashughulikia waamini walioko Amerika Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Canada.[3]
Kadiri ya Annuario Pontificio ya mwaka 2016, mwishoni mwa mwaka 2012 Kanisa hilo lilikuwa na waamini 504,280 katika parokia 1225, wakiongozwa na maaskofu 8 na mapadri wanajimbo 882 hivi, ingawa sensa iliyoendeshwa na serikali ya Romania mwaka 2011 ilidai waamini waliokuweko nchini walikuwa 150,593 tu.[4][5]
Historia
haririBaada ya Austria kuteka Transilvania mwaka 1687, askofu mkuu Atanasie Anghel alikubali kuungana na Kanisa la Roma mwaka 1698, na uamuzi huo ulipitishwa na sinodi ya maaskofu tarehe 4 Septemba 1700.[6]
Baada ya Ukomunisti kuteka Romania, ulilazimisha waamini wote wa Kanisa hilo kujiunga tena na Waorthodoksi, lakini wengine walikataa na kuendelea kufuata imani yao kwa chinichini, bila ya kujali dhuluma iliyoendelea hadi tarehe 31 Desemba 1989.
Viungo vya nje
hariri- "Biserica Română Unită cu Roma, Greco-Catolică" (in Romanian)
- Another informative site (in Romanian) Archived 21 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.
- Another informative site (in Romanian) Archived 25 Juni 2013 at the Wayback Machine.
- "Romanian Greek Catholic community in Madrid, Spain (Web)" (in Romanian and Spanish) Archived 11 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- "Romanian Greek Catholic community in Madrid, Spain (Blog)" (in Romanian and Spanish)
- "Chiesa Romena Unita con Roma, Greco-Cattolica" (in Italian) Archived 1 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
- St. George Romanian Byzantine Catholic Diocese (in English)
- Article on the Romanian Greek Catholic Church by Ronald Roberson on the CNEWA website. Archived 10 Julai 2009 at the Wayback Machine.
- Radio Free Europe/Radio Liberty: The Romanian Orthodox Church and Post-Communist Democratization*Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
- Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
- [1] Archived 5 Machi 2012 at the Wayback Machine. - Hati ya Papa Yohane Paulo II Orientale Lumen kuhusu Makanisa ya Mashariki
- Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki (katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba)
- Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Archived 25 Aprili 2009 at the Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
- Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo Archived 17 Mei 2011 at the Wayback Machine.
- CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo Archived 9 Machi 2009 at the Wayback Machine.
- Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
- Takwimu za Makanisa hayo Archived 27 Juni 2007 at the Wayback Machine.
Tanbihi
hariri- ↑ Source: http://recensamant.referinte.transindex.ro/ Archived 20 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- ↑ "Romanian Catholic site". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-23. Iliwekwa mnamo 2013-07-07.
- ↑ Romanian Catholic Eparchy of St George's in Canton
- ↑ 2002 Romanian census official data.
- ↑ International Religious Freedom Report 2005 United States Department of State
- ↑ The Harper Collins Encyclopedia of Catholicism (New York: Harper Collins, 1995) 1132.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |