Kanuni ya kitawa
Kanuni ya kitawa ni maandishi ya kiroho yanayokusudiwa kuongoza hata kisheria maisha ya wamonaki au watawa wengine.
Kanuni ileile inaweza kuongoza shirika moja tu au mengi, kama vile Kanuni ya Ndugu wa Kiume na wa Kike wa Utawa Hasa wa Tatu wa Mt. Fransisko, inayofuatwa na mashirika karibu 400 duniani kote, yakiwa na jumla ya watawa 200,000 hivi.
Mwandishi wa kanuni kwa kawaida ni mtakatifu aliyeitunga ili kushirikisha karama yake kama mwanzilishi.
Kati ya kanuni za zamani zilizo maarufu zaidi, ziko zile za Pakomi, Basili Mkuu, Benedikto wa Nursia, Kolumbano na Fransisko wa Asizi.
Mwanamke wa kwanza kuandika kanuni ya kitawa alikuwa Klara wa Asizi (1253).
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanuni ya kitawa kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |