Kariobangi

Kariobangi ni mtaa wa Nairobi ulio kata ya tarafa ya Kasarani. Iko upande wa mashariki wa Nairobi kati ya Dandora na Huruma. Kuna Kariobangi North na Kariobangi South; nyumba ziko za ghorofa lakini kuna pia maeneo ya mabanda.

Mtaa huu unajulikana sana kwa malori ya kusafirisha vifaa vya ujenzi kama vile changarawe, mawe na kadhalika.