Kasam Paida Karne Wale Ki
Kasam Paida Karne Wale Kini filamu iliyotoka mwaka 1984 ya lugha ya [[Kihindi]. Filamu imetayarishwa na kuongozwa na Babbar Subhash. Ndani yake anakuja Mithun Chakraborty, Smita Patil, Salma Agha, Karan Razdan, Geeta Siddharth na Amrish Puri.
Kasam Paida Karne Wale Ki | |
---|---|
Imeongozwa na | Babbar Subhash |
Imetayarishwa na | Babbar Subhash |
Nyota | Mithun Chakraborty Smita Patil Salma Agha Amrish Puri |
Muziki na | Bappi Lahiri |
Imesambazwa na | B. Subhash Film Unit |
Imetolewa tar. | Novemba 30, 1984 |
Nchi | India |
Lugha | Kihindi |
Hadithi
haririKasam Paida Karne Wale Ki ni hadithi inayomhusu Satish Kumar (Mithun Chakraborty). Baada ya kifo cha baba yake, Satish anabaki kuwa mrithi pekee wa shamba kubwa kabisa. Kwa vile ana miaka mitano tu, anaruhusiwa kurithi mazima hadi afikapo miaka 20. Shamba hilo lipo chini ya uangalizi wa babake mkubwa, Udaybhan Singh (Amrish Puri), ambaye anamtisha kupindukia mtoto wa kakake kiasi kwamba anaogopa hata kivuli cha babake mkubwa.
Miaka inaenda. Satish anautwaa ukubwa, kamwoa Aarti (Smita Patil), huku bado anaishi maisha ya kumuogopa babake mkubwa. Baada ya usiku mmoja wa furaha, Satish anagundua ya kwamba Aarti alikubali kuolewa nae ili aweze kumwibia fedha taslimu na mikufu ya dhahabu. Anavurugwa. Uday anamtaka Aarti aondoke, halafu Satish anamfuata. Aarti anamwomba msamaha, anamsamehe. Hata hivyo, Udaybhan anampiga kisu cha tumbo hadi kufa na kwenda kuandikisha polisi kama jamaa amaejinyonga. Aarti anaapa kulipiza kisasi kupitia mtoto wake aliyetumboni. Miaka inaenda, Aarti na mtoto wake wa kiume, Avinash (Mithun Chakraborty), anaibuka kulipiza kisasi cha kifo cha Satish — wanagundua sio rahisi kumkaanga Udaybhan, na katika kufanikisha suala zima la kisasi huenda pia likapelekea kuhatarisha maiasha yao.
Washiriki
hariri- Mithun Chakraborty as Satish Kumar / Avinash S. Kumar
- Smita Patil kama Aarti S. Kumar
- Salma Agha kama Leena
- Amrish Puri kama Udaybhan Singh
- Gita Siddharth kama Satish's Daimaa
- Jagdish Raj kama Judge
- Karan Razdan kama Chanderbhan U. Singh
- Master Subramanium kama Mithun Chakraborty mtoto
- Bob Christo kama Msaidizi wa Udaybhan