Kaunti ya Mombasa
Kaunti ya Mombasa imeshika nafasi ya wilaya ya Mombasa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Kaunti hii ni mojawapo ya kaunti mbili ambazo pia ni jiji na ndio kaunti ndogo kabisa kati ya kaunti zote.
Kaunti ya Mombasa Kaunti 001 | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
| |||||
Utangamano kwa maendeleo | |||||
Mombasa County in Kenya.svg Kaunti ya Mombasa katika Kenya | |||||
Coordinates: 4°03′S 39°40′E / 4.050°S 39.667°E | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 1 | ||||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani | ||||
Makao Makuu | Mombasa | ||||
Gavana | Hassan Ali Joho | ||||
Naibu wa Gavana | Dkt. William Kingi | ||||
Seneta | Mohammed Faki | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Asha Hussein Mohammed | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Mombasa | ||||
Spika | Arub Ibrahim Khatri | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 30 | ||||
Mahakama | Mahakama ya Rufaa, Mombasa | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 6 | ||||
Eneo | km2 219.9 (sq mi 84.9) | ||||
Idadi ya watu | 1,208,333 | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 5,495 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | mombasa.go.ke |
Inapakana na kaunti za Kwale na Kilifi ambazo pamoja na kaunti za Mombasa, Lamu, Tana River na Taita Taveta zilikuwa zinatengeneza Mkoa wa Pwani.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,208,333 katika eneo la km2 219.9, msongamano ukiwa hivyo wa 5,495 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu ya serikali ya kaunti yako katika jiji la Mombasa.
Jiografia
haririKaunti ya Mombasa inapakana na Bahari Hindi. Ina kisiwa cha Mvita ambacho huwa kati mwa Jiji la Mombasa. Kimetenganishwa na bara na Kijito cha Tudor na Kijito cha Port Reitz[2]. Vijito hivyo hugawanywa na Makupa Causeway. Maeneo hayo mengine ya bara yameunganishwa kwa feri na daraja. Ardhi yake ni tambarare.
Lindi la Bandari ya Kilindini, lenye kina cha mita 45-55, huiwezesha kuegeshwa meli kubwa[3].
Mombasa ina misitu asilia mitatu ambayo ni 6% ya misitu ya mikoko ya Kenya[4]. Misitu hiyo ni mojawapo ya makazi ya wanyamapori katika kaunti hii. Hata hivyo, uvunaji kupindukia wa miti, maeneo taka na kupanua ardhi baharini kumeharibu misitu hii na kuathiri wanyamapori wa majini na ardhini[5][6].
Kaunti ya Mombasa ina tabianchi ya tropiki[7]. Kwa kuwa iko kando na bahari, kiwango cha unyevuanga huwa juu. Hali ya hewa hutegemea pepo za monsuni. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Juni na Oktoba hadi Disemba.
Kubadilika kwa wastani wa hali ya hewa kumesababisha kiwango cha upwaji wa bahari kupanda na kuongezeka kwa halijoto, mambo ambayo yanatishia jiji la Mombasa na turathi ya Fort Jesus. Pia, mafuriko ya pwani, mmomonyoko katika fuko na kutoweka kwa mwamba tumbawe kumesababishwa na mabadiliko haya[8][9][5].
Uchumi
haririUchumi wa Mombasa na nchi ya Kenya kwa jumla hutegemea sana bandari ya Mombasa. Bandari ya Mombasa ndio bandari kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Bidhaa nyingi hupitia hapo kutoka na kuingia ndani ya nchi. Bandari hii pia hutegemewa na nchi ya Uganda, Burundi, Sudani Kusini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kupitisha bidhaa kama vile, mafuta[10].
Mombasa pia ni kituo kikuu cha utalii kwa sababu ya fuko zake zenye mchanga, Fort Jesus na Mji wa Kale. Baada ya mashambulizi kadhaa ya kigaidi katika miaka ya awali ya mwongo wa 2010 na Al Shabaab na vikundi vingine, utalii ulidorora[11][12]. Nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa pamoja na nchi zingine za magharibi zilianza kutoa tahadhari za safari. Baada ya Operesheni Linda Nchi, na juhudi za polisi kukumbana na ugaidi, juhudi zinaelekezwa kuimarisha utalii tena[13]. Pia, kuanzishwa kwa huduma ya reli mpya ya SGR kati ya Jiji la Mombasa na Nairobi, kumeongeza idadi ya watalii wa ndani[14].
Mnada wa Chai wa Mombasa ni mojawapo ya vituo vya unadi wa chai katika dunia. Mnada huu hunadi chai kutoka nchi za Kenya, Tanzania, Uganda Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Madagaska, Zambia na Zimbabwe. Kufikia mwaka wa 2017, ulikuwa soko ya pili kwa ukubwa ya uuzaji wa chai katika dunia[15].
Maeneo bunge
haririKaunti ya Mombasa ina maeneo bunge yafuatayo[16]:
Kaunti ndogo/Eneo bunge | Kata |
---|---|
Changamwe | Port Reitz, Kipevu, Airport, Changamwe, Chaani |
Jomvu | Jomvu Kuu, Miritini, Mikindani |
Kisauni | Mjambere, Junda, Bamburi, Mwakirunge, Mtopanga, Magogoni, Shanzu |
Nyali | Frere Town, Ziwa la Ngombe, Mkomani, Kongowea, Kadzandani |
Likoni | Mtongwe, Shika Adabu, Bofu, Likoni, Timbwani |
Mvita | Mji wa Kale/Makadara, Tudor, Tononoka, Majengo Ganjoni/Shimanzi |
- Changamwe 131,882
- Jomvu 163,415
- Kisauni 291,930
- Likoni 250,358
- Mvita 154,171
- Nyali 216,57
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ www.knbs.or.ke
- ↑ Sant Bahadur Singh (1995). Emerging Frontiers of Urban Settlement Geography. M.D. Publications Pvt. Ltd. ku. 97–. ISBN 978-81-85880-83-9.
- ↑ "Port of Mombasa, Kenya Archived 8 Julai 2018 at the Wayback Machine.". www.findaport.com. Shipping Guides Ltd. Retrieved 18 March 2018.
- ↑ "NATIONAL MANGROVE ECOSYSTEM MANAGEMENT PLAN" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-05-17. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
- ↑ 5.0 5.1 Atieno, Winnie. "Mombasa getting hotter as mangroves rapidly disappear from coastline - Business Daily". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
- ↑ Mghenyi, Charles. "Waste, sea reclamation kill Mombasa mangroves, destroy forests". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
{{cite web}}
: Text "The Star, Kenya" ignored (help) - ↑ "CLIMATE: MOMBASA", Climate-Data.org, ilipatikana 13-04-2013
- ↑ Olingo, Allan. "East Africa's coast is slowly sinking - The East African". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
- ↑
Agutu, Nancy. "Climate doom: Rising seas, submerged hotels, thousands jobless". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
{{cite web}}
: Text "The Star, Kenya" ignored (help) - ↑ "History of The Port Of Mombasa", Halmashauri ya Bandari za Kenya, ilipatikana 13-04-2018
- ↑ "10 wajeruhiwa katika shambulio Kenya", BBC Kiswahili, ilipatikana 13-04-2018
- ↑ "GRENADE ATTACK KILLS ONE IN MOMBASA NIGHT CLUB Archived 2012-09-11 at Archive.today". The Star. 16 May 2012. Retrieved 31 May 2012.
- ↑ Charles Wasonga, "Serikali ikomeze utovu wa usalama kupiga jeki utalii", Taifa Leo, ilipatikana 13-04-2018
- ↑ Philip Mwakio, "Wildebeest migration and SGR boost tourism", The Standard, ilipatikana 13-04-2018
- ↑ GERALD ANDAE, "Mombasa tea sale records third best price globally", Business Daily, ilipatikana 13-04-2013
- ↑ http://countytrak.infotrakresearch.com/Mombasa-county/
- ↑ www.knbs.or.ke
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Mombasa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |