Kelvin Kiptum Cheruiyot alikuwa mwanariadha wa mbio za marathoni. Amekufa mwezi wa mbili mwaka 2024[1], lakini yeye bado anakuwa na rekodi ya dunia kwa mbio za marathoni. Yeye ni mtu mmoja tu aliyekimbia haraka kuliko masaa mawili na dakika moja.

Familia hariri

Kelvin Kiptum alizaliwa tarehe mbili mwezi wa kumi na mbili mwaka 1999. Aliishi katika kijiji cha Chepsamo nchi ya Kenya. Kuna wanariadha wa mbio za kukimbia wengi wanayetoka eneo hii. Kiptum alikuwa mtoto pekee wa Samson Cheruiyot, baba yake.[2] Alipokuwa mtoto, yeye alifanya kazi nyingi kwa familia yake, na alianza kukimbia kwa sababu alichunga ng’ombe kijijini kwake.

Kazi hariri

 

Kiptum alipokuwa na miaka kumi na tatu mwaka 2013, alianza kukimbia katika mashindano la mbio; alikimbia mbio za marathoni ya nusu, na akashika nafasi ya kumi. Aliendelea kukimbia katika mbio za marathoni ya nusu hizi kila mwaka, na alishinda mbio za marathoni ya nusu mwaka 2018. Mwaka 2019 alianza kushindana mbio za marathoni ya nusu za mataifa.[3] Alisafiri mji wa Lisbon nchi ya Ureno kwa kukimbia katika Lisbon Half Marathon, na akashindia nafasi ya tano. Mwaka huo, alishiriki mbio saba katika Ulaya, na aliporudi nchi yake Kenya, alishinda Kass Half Marathon mwezi wa kumi na moja. Mpaka mwaka 2020, Kiptum hakuwa na mkufunzi, lakini mwaka 2020 Gervais Hakizimana alianza kumfundisha kwa sababu Kiptum alitaka kushinda mbio za marathoni kamili.

  1. Mather, Victor (2024-02-13), "Kelvin Kiptum, Marathon World Record-Holder, Is Dead at 24", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2024-04-24 
  2. https://www.the-star.co.ke/authors/magdaline-saya. "Strange people looked for him 4 days before his death - Kiptum's father speaks". The Star (kwa en-KE). Iliwekwa mnamo 2024-04-24. 
  3. "Kelvin KIPTUM | Profile | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2024-04-24.