Kenya Ports Authority
Kenya Ports Authority (kifupi: (KPA)) ni shirika la serikali la Kenya lenye wajibu wa "kudumisha, kutekeleza, kuboresha na kusimamia kufanyika kwa huduma zote kwenye Bahari ya Hindi ukanda wa pwani ya Kenya, ikiwa ni pamoja na Bandari ya Kilindini hususan ya Mombasa. Bandari zengine zinazohudumiwa na KPA ni pamoja na Lamu, Malindi, Kilifi, Mtwapa, Kiunga, Shimoni, Funzi na Vanga. KPA ilianzishwa mwaka wa 1978 kwa kitendo cha Bunge na iko Mombasa.[1][2]
Kenya Ports Authority ni mwekezaji asili katika shirika la serikali ya Kenya, Kenya National Shipping Line, ambayo ilianzishwa mwaka wa 1989.[3]
Katika mwaka wa 1989, serikali ya Kenya ilileta pamoja uendeshaji na udhibiti wa huduma zilizokuwa za feri, ikiwemo pamoja na Likoni Ferry service hapo Likoni, Mombasa, zote zikawa katika hidara moja ya KPA, Kenya Ferry Services. Hidara hiyo ilitunukiwa hadhi ya hali ya shirika la serikali ya Kenya lenye uwezo wa kujitegemea mnamo mwaka wa 1998.[4]
KPA pia inamiliki timu za michezo mbalimbali, ikiwemo timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, Bandari FC pamoja na klabu ya timu mojawapo ambayo huongoza mpira wa kikapu ya wanawake.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kenya Ports Authority kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "kPa, Kuhusu sisi, Mandate". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-22. Iliwekwa mnamo 2009-11-29.
- ↑ "Serikali ya Kenya, State Corporations, Kenya Ports Authority". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-19. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
- ↑ "Kenya National Shipping Line, Kuhusu sisi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-04. Iliwekwa mnamo 2009-11-29.
- ↑ "Kenya Ferry Services, Historia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-14. Iliwekwa mnamo 2009-11-29.