Keremoni na wenzake

Keremoni na wenzake (walifariki katikati ya karne ya 3) walikuwa Wakristo wa Misri waliokimbia dhuluma ya kaisari Decius dhidi yao.

Dionisi wa Aleksandria, katika barua kwa Fabio wa Antiokia [1] iliyoripotiwa na Eusebi wa Kaisarea pia [2], alishuhudia ushujaa wa wafiadini na kusikitikia kifo cha wengi walipokimbilia jangwani au milimani, kati yao askofu mzee Keremoni wa Nilopoli na mke wake[3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 22 Desemba[4][5].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. PG, X, 1306
  2. Hist. Eccl., VI, 41, katika PG, XX, 605-12
  3. Eusebio, VI, 42, PG, XX, 614
  4. Martyrologium Romanum
  5. https://catholicsaints.info/saint-chaeremon-of-nilopolis/
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.