Khumbize Chiponda
Khumbize Kandodo Chiponda ni mwanasiasa wa Malawi. Mnamo mwaka wa 2020 alikua Waziri wa Afya nchini Malawi.
Khumbize Chiponda ni dada wa Ken Kandodo, pia mwanasiasa, na ana uhusiano na rais mwanzilishi wa Malawi, Hastings Banda. Kabla ya kuingia kwenye siasa alifuzu kama mfamasia, na alifanya kazi katika Wizara ya Afya kama mtaalamu wa biokemikali.[1]
- ↑ Joshua Malango. "Germany commits to support Malawi health sector", 24 July 2020.