Kibahonsuai ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabahonsuai kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kibahonsuai imehesabiwa kuwa watu 200 tu. Kwa vile Wabahonsuai wengi wameshaanza kuacha lugha yao, Kibahonsuai imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibahonsuai iko katika kundi la Kicelebiki.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibahonsuai kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.