Kabomo Vilakazi

Muigizaji na mwanamuziki wa Afrika Kusini
(Elekezwa kutoka Kibomo vilakazi)

Kabomo Vilakazi (anafahamika kwa jina la Kabomo; alizaliwa Benoni, Gauteng, Afrika ya Kusini, 27 Julai 1978) ni mwigizaji wa Afrika ya Kusini. Anajulikana katika uhusika wake katika filamu na sinema za kwenye runinga kama Zabalaza, sink na Seriously Single [1]. Mbali na uigizaji kabomo ni mhariri, mwandishi, msomaji, mwimbaji na pia ni msimamizi wa sanaa[2][3]

Kabomo Vilakazi
Amezaliwa Kabomo Vilakazi
27 Julai 1978)
alizaliwa Benoni, Gauteng, Afrika ya Kusini.
Jina lingine Kabomo
Kazi yake Mwigizaji wa Afrika ya Kusini.

Wimbo wa kwanza wa Kabomo "Uzobuya", ulichapishwa mwaka 2012. Mafanikio yake yalitokana na albamu mbili ambazo ni All Things Grey and Sekusile.[4] Katika sinema ya Zabalaza Kibomo aliigiza sehemu ndogo na ikamfanya apate nafasi ya kuwa mwigizaji mkuu kwenye sinema ya Vuzu sitcom Check Coast mwaka 2014.[2] Mnamo mwaka 2015 kabomo alionekana katika filamu ya sink na kwenye mfululizo wa sinema ya Sober Companion na kwenye maonyesho maarufu kama Soul City, Scandal, Thola, Saints & Sinners, Umlilo, Captain Bozaa na Tshisa. [1]

Kama mtunzi aliandika nyimbo nyingi kwa waimbaji kama Tshepo Tshola, Unathi, Aya, Kelly Khumalo, Thiwe, Nothende, Flabba, The Fridge, Flatoe, Pebbles, Zubz, Dineo Moeketsi.[2] Pia aliongoza filamu mbili nazo ni Droplets na Melody. Wakati akiongoza filamu pia aliandika hati ya sinema maarufu katika maonyesho ya sepedi SABC1 ijulikanayo kama Skeem Sam.[1] Hata hivyo, baadaye alilaumiwa na wafanyakazi wa filamu ya "Droplets" kwa kusema kwamba hakuweza kulipa.[5]

Ilipofika mwezi 8 2020 aliigiza kwenye filamu ya kuchekesha ya Seriously Single ikiongozwa na Katleho Ramaphakela na Rethabile Ramaphakela.[6] Ilitolewa na kuonyeshwa 31 Julai 2020 kwenye Netflix.

Uhusika wa vipindi vya runinga

hariri
  • Check Coast kama Bheka Zonke
  • Rhythm City kama Robert
  • Generations kama Pastor Zondo
  • Scandal kama Doctor Ndaba
  • Zabalaza kam Herbert
  • Sober Companion kama KG
  • The Republic kama Minister of Finance
  • The Mayor kama Pastor
  • Thola kama Sam
  • Jozi Street kama Dingaan

Filamu zake

hariri
Mwaka Filamu Uhusika Aina.
2015 Sink Taxi driver Filamu
2020 Seriously Single Pastor Filamu

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Kabomo Vilakazi: Personal Biography". legends. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-17. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2020. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Kabomo Vilakazi: Born: 27 July 1978 (42 years old)". tvsa. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Kabomo Vilakazi – My friends have turned on me". news365. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Kabomos happy where he is!". Daily Son. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Droplets stars still not paid, four years after producer Kabomo released film". Sowetan Live. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Seriously Single's Bohang Moeko and Yonda Thomas reflect on love and dating". news24. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabomo Vilakazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.