Nyaraka za kigezo[mtazamo] [hariri] [historia] [safisha]

Unaweza kuonyesha anwani ya kijiografia (pia majiranukta, ing. coordinates) juu ya makala ya mji, jengi au mahali pengine na kuitazama kwenye ramani kwa kugonga tu.

Kuna namna mbili za kuandika majiranukta:

  1. kwa kutaja nyuzi, dakika na sekunde
  2. kwa namna ya desimali

Umbo la nyuzi-dakika-sekunde

Unaweza kutafuta anwani hii kwa mfano kutoka google earth. Kwa mfano unafungua google earth, unaweka "marker" njano katika eneo la mji wa Kairo, Misri. Majiranukta za marker hii ni: 29°58'45.78"N 31° 8'4.92"E. Utakumbuka tarakimu pale, halafu utanakili mstari wa mfano hapo chini na kubadilisha tarakimu ipasavyo, halafu ingiza katika makala.

Tahadhari: ukichukua kutoka google earth utumie sehemu tatu za kwanza pekee, acha sehemu za sekunde yaani nukta na tarakimu baadaye (hapo juu utatumia tarakimu zinazoonekana koze pekee)

{{Coord|29|58|45|N|31|8|4|E|display=title}}

Mfano huu unatumia anwani inayoonyeshwa kwa nyuzi, dakika na sekunde. Utaichukua kutoka Google Earth kwa kuweka marker njano mahali penyewe halafu unaweza kuona namba za anwani kwa kuangalia tabia za marker.

Sehemu ya mwisho "display=title" acha ilivyo.

Umbo la desimali

Kuna pia programu za ramani zinazoonyesha anwani kwa namna ya desimali, kwa mfano Google Maps. Unabofya right-click na "What is here", unaona tarakimu za anwani. Au kwenye simu yako unaacha kidole kwa muda dirishani hadi unaona mshale mwekundu pale ulipoweka kidole. Dirisha la juu la simu inaonyesha tarakimu ambazo ni viwianisha vya desimali. Halafu utumie mfano hapo chini kwa anwani 29.979571,31.134668 :

{{Coord|29.979571|31.134668|display=title}}

Utabadilisha tarakimu ipasavyo. Usisahau alama ya - (kasoro) ikitokea! Hii inafanya tofauti baina ya kaskazini na kusini ya ikweta.