Onyo dhidi ya kuandika juu ya kazi ya wengine bila taarifa

Ulichangia makala katika wikipedia hii. Asante sana! Kwa bahati mbaya ulichagua kichwa kilichokuwepo tayari. Ukitumia google-translate labda hujatambua ya kwamba uliweka tafsiri yako juu ya makala iliyopo tayari.

Ni sawa kabisa ukibadilisha makala, au kuongeza mambo ndani yake.

Mara chache ni afadhali kufuta yote. Ila tu hapa kwenye wikipedia tunajadiliana kabla ya kufuta kazi ya wengine. Kuna ukurasa wa majadiliano unapoweza kutaja sababu kwa nini makala jinsi ilivyo si nzuri halafu subiri siku 2 hadi kufanya mabadiliko makubwa. Unaweza pia kiuangalia historia ya makala na kumwandikia mchangiaji aliyetangulia moja kwa moja.

Haikubaliki kufuta kazi ya wengine kimya-kimya. Hata kama hujakusudia kufanya hivyo tulilazimishwa kufuta kazi yako na kurejesha hali ya awali. Uko huru kuchukua sehemu za maandishi yako na kupeleka kama nyongeza katika makala iliyopo.