Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyonakiliwa kutoka tovuti nyingine. Kiasi cha matini uliyokopi ni kikubwa mno, tena hujaionyesha kuwa nukuu kutoka chanzo chake.

Uliarifiwa kwamba ni mwiko kuleta matini au picha kutoka tovuti za nje. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Maelezo hariri

Mkabidhi (si mtumiaji wa kawaida) anaweza kutumia kigezo hiki baada ya kumzuia mchangiaji aliyekuwa na kosa la kuleta maudhui kutoka tovuti nyingine kwa njia ya kopi-paste.

Nakili sehemu hiyo {{zuia tafsiri}} ~~~~ na uiweke kwenye ukurasa wa mhusika. Afadhali weka pia jina la makala ambayo / ambazo ni sababu ya kumzuia kwa kuandika [[JINA LA MAKALA]] kabla ya alama ya ~~~~.

Akikubali kusafisha makala zake tumrudishe lakini tuzidi kumfuatilia.