Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Maelezo

Mkabidhi (si mtumiaji wa kawaida) anaweza kutumia kigezo hiki baada ya kumzuia mchangiaji aliyekuwa na kosa la kumwaga tafsiri ya kompyuta bila kusahihisha kwa kutosha.

Nakili sehemu hiyo {{zuia tafsiri}} ~~~~ na uiweke kwenye ukurasa wa mhusika. Afadhali weka pia jina la makala ambayo / ambazo ni sababu ya kumzuia kwa kuandika [[JINA LA MAKALA]] kabla ya alama ya ~~~~.

Tuwe macho kabla ya kumzuia mchangiaji. Kosa moja dogo lisiwe sababu ya kutosha. Lakini tukiona sentensi 3 ambazo hazieleweki vema au kama tumechunguza hali kwa kuweka makala iliyotafsiriwa (kwa kawaida kutoka en.wiki) katika dirisha la translate.google.com na kuthibitisha matini ya makala imetokea hapa, tuna sababu ya kutosha.

Akikubali kusafisha makala zake tumrudishe lakini tuzidi kumfuatilia. Tunaweza kumwekea masharti ya kuhariri kwa muda katika nafasi yake ya mumiaji pekee (user space) ili michango yake yaangaliwe kwanza kabla ya kuihamisha katika nafasi ya makala (main space9 kama makala kamili