Kisirili

(Elekezwa kutoka Kikirili)

Kisirili ni aina ya mwandiko au alfabeti inayotumiwa kuandika lugha mbalimbali za Ulaya ya Mashariki na Asia ya Kati, kwa mfano Kirusi, Kiserbia, Kitajiki.

Mwandiko kwa ajili ya lugha za Kislavoni

hariri

Jina limetokana na mmonaki na mtaalamu Mgiriki Mt. Sirili (827 - 14 Februari 869) aliyesemekana aliunda namna hiyo ya mwandiko kwa ajili ya lugha za Kislavoni pamoja na mdogo wake Mt. Methodio.

Hali halisi hawakuanzisha aina hii ya alfabeti lakini waliendeleza namna ya kuiandika iliyosaidia kusambaza mwandiko kati ya mataifa wasemaji wa lugha za Kislavoni. Lugha hizo zina sauti kadhaa ambazo hazina herufi katika alfabeti ya Kilatini. (Mwandiko wa Kilatini hutumiwa siku hizi kwa lugha nyingi duniani, zikiwa pamoja na Kiswahili na Wikipedia hii.)

Kuna lugha za Kislavoni, kama vile Kipoland, Kicheki na Kikroatia, zinazoandikwa kwa alfabeti ya Kilatini, lakini kuna alama za nyongeza kwa ajili ya sauti za pekee za lugha za Kislavoni kwa mfano: "Č" kwa sauti ya "tsh" au "Ž" kwa aina ya "sh laini".

Alfabeti za Kisirili zinatofautiana kiasi kati ya lugha na lugha; kuna namna tofauti za kuandika sauti ileile au pia herufi za pekee kwa ajili ya sauti za pekee katika lugha fulani. Alfabeti inayotumiwa na watu wengi ni ya Kirusi inayoonyeshwa hapa.

Lugha za Kislavoni zinazoandikwa kwa alfabeti ya Kisirili ni:

Mwandiko wa lugha za Kiasia

hariri

Kutokana na athira ya Urusi katika Asia ya Kati kuna pia lugha mbalimbali za Kiasia ambazo zinaandikwa kwa mwandiko wa Kisirili tangu karne ya 19 au mwanzo wa karne ya 20. Nchi zinazohusika zilikuwa ama sehemu za Umoja wa Kisovyet au nchi jirani kama Mongolia.

Lugha kadhaa za Kiasia zinazoandikwa siku hizi kwa alfabeti za Kisirili ni:

Mfano wa alfabeti ya Kirusi

hariri
Herufi za Kisirili
(kubwa / ndogo)
Herufi za Kilatini zinazolingana Matamshi
А а A a a baba wangu
Б б B b b baba
В в V v v vitabu
Г г G g g (w) gani, na uhuru kwa kiukraine
Д д D d d dada, ndogo
Е е E e e / ye Kwa kirusi: yeye. Kwa lugha si kirusi: yeye.
Ё ё Ë ë yo Yohane
Ж ж Ž ž sh laini kiingereza vision, Kifaransa je
З з Z z z maziwa
И и I i i kiswahili
Й й J j i fupi yeye
К к K k k kaka
Л л L l l lakini, italiki
М м M m m maziwa, mtoto, damu
Н н N n n nani
О о O o o mtoto, kifaransa l'eau
П п P p p pole
Р р R r r rafiki
С с S s s sisi
Т т T t t mtoto
У у U u u uhuru
Ф ф F f f safari, fisi, rafiki
Х х Kh kh kama matamshi ya Kiarabu
"Alkhamisi" (Alhamisi) subulkheri
Ц ц C c ts kijerumani Zehn, kiitalia pizza,
Ч ч Č č tsh (ky) chumba, kiingereza chair
Ш ш Š š sh shamba
Щ щ Ŝ ŝ shtsh/kipoland szcz~śś: ɕ:
Ъ ъ " (alama gumu) alama hii hunonyesha matamshi
„magumu“ ya herufi inayotanguulia
Ы ы Y y Y y [ɨ],[ʉ]; kiingereza cha Marekani roses
Ь ь (alama laini) alama hii huonyesha sauti
ya "y" baada ya herufi vyakula?
Э э È è e fupi ndege, kijerumani Zehn
Ю ю Û û yu yunifomu, kiingereza useful
Я я Â â ya yangu