Kikwamba (kutoka kitenzi kwamba, chenye maana ya kusema au kunena) ni aina ya shairi (bahari) ambalo neno la kipande cha kwanza katika kila mshororo hujirudiarudia katika ubeti [1], kwa mfano:

Kusema yanilazimu, daima sitonyamaza

Kusema yanilazimu, kimya kina nichukiza

Kusema yanilazimu, kipo cha kuwaeleza

Kama kusema ugonjwa, basi niache niumwe.

Tanbihi

hariri
  1. "Bahari za Ushairi | Paneli la Kiswahili". swa.gafkosoft.com. Iliwekwa mnamo 2020-01-30.
  Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikwamba kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.