Kipanya mnono
Kipanya mnono wa Krebs (Steatomys krebsii) aliyekufa
Kipanya mnono wa Krebs (Steatomys krebsii) aliyekufa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Nesomyidae (Wanyama walio na mnasaba na buku)
Forsyth Major, 1897
Nusufamilia: Dendromurinae (Wanyama wanaofanana na vipanya-miti)
Alston, 1876
Jenasi: Steatomys
Peters, 1846
Ngazi za chini

Spishi 8:

Vipanya wanono ni wanyama wadogo wa jenasi Steatomys katika nusufamilia Denromurinae wa familia Nesomyidae ambao wanafanana na vipanya, lakini vipanya wa kweli ni wanafamilia wa Muridae. Spishi zote zinatokea mahali pengi pa Afrika kusini kwa Sahara, katika maneneo ya manyasi hasa. Rangi yao ni kijivu hadi kahawia, lakini tumbo ni jeupe. Vipanya hawa ni wafupi na wanono; mkia una urefu sawa kuliko mwili. Mwili wao una hazina kubwa za mafuta. Kwa hivyo huliwa sana mahali pengi pa Afrika. Kinyume na vipanya-miti vipanya wanono huishi ardhini hasa.

Spishi

hariri

References

hariri
  • Kingdon, J. 1997. The Kingdon Field Guide to African Mammals. Academic Press Limited, London.
  • Musser, G. G. and M. D. Carleton. 2005. Superfamily Muroidea. Pp. 894-1531 in Mammal Species of the World a Taxonomic and Geographic Reference. D. E. Wilson and D. M. Reeder eds. Johns Hopkins University Press, Baltimore.
  • Steppan, S. J., R. A. Adkins, and J. Anderson. 2004. Phylogeny and divergence date estimates of rapid radiations in muroid rodents based on multiple nuclear genes. Systematic Biology, 53:533-553.