Kirukanjia wa Afrika

Kirukanjia wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Soricomorpha (Wanyama kama virukanjia)
Familia: Soricidae (Virukanjia)
G. Fischer, 1817
Nusufamilia: Myosoricinae (Virukanjia wa Afrika)
Kretzoi, 1965
Jenasi: Congosorex Heim de Balsac & Lamotte, 1956

Myosorex Gray, 1838
Surdisorex Thomas, 1906

Virukanjia wa Afrika ni wanyama wadogo wa nusufamilia Myosoricinae katika familia Soricidae wanaofanana na vipanya, lakini virukanjia si wagugunaji (oda Rodentia). Spishi hizi zinatokea Afrika kusini kwa Sahara tu lakini hawa si spishi pekee za Afrika. Kuna spishi nyingi nyingine za virukanjia katika Afrika walio wanafamilia wa nusufamilia Crocidurinae (virukanjia meno-meupe). Hula wadudu na nyungunyungu hasa lakini mbegu na makokwa pia. Meno yao yamechongoka yenye ncha kali. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia.

SpishiEdit