Kisaka ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana katika baadhi ya viji vya maeneo ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliosambaa katika vijiji vingi kidogo vya himaya kadhaa za katikati kuelekea mashariki ya Kilimanjaro.

Ukoo wa Kisaka umesambaa ndani na nje ya Tanzania wakiwa wanafanya vizuri katika nyanja mbalimbali hususan kitaaluma na hata kwenye utumishi wa umma. Japo sio ukoo mkubwa sana lakini ni ukoo uliojitofatisha na wenye mshikamano mkubwa baina ya wanaukoo ukiwa ni ukoo wa watu makini na wenye nmsimamo mkali.

Wachagga wa ukoo wa Kisaka wameendelea kuongeza idadi katika maeneo ya vijiji wanakopatikana lakini huenda chimbuko au asili yake ikawa Kirua Vunjo kwani ndiko wanakopatikana kwa wingi zaidi. Hata hivyo katika maeneo ya vijiji vya Old Moshi wanapatikana kwa wingi kiasi pia.

Hivyo ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyaseni, Uru. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Maruwa, Kirua Vunjo Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi sana kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Leghomulo, Kilema. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema. Ukoo wa Kisaka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Makami Juu, Kilema. Ukoo wa Kisaka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Makami chini, Kilema. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa kiasi kijiji cha Kotela, Mamba. Ukoo wa Kisaka wanapatikana kwa uchache kijiji cha Kirisha, Sanya Juu.

Marejeo

hariri

1. Sebastian Moshi, Ukoo wa kisaka (https://www.facebook.com/100003111954681/posts/6395948630518805/?app=fbl)
2. Sebastian Moshi, Miaka 700 ya Wachagga