Kisilesia
Kisilesia (kwa Kisilesia: ślůnsko godka, ślůnski, pia huitwa pů našymu) ni lugha izungumzwayo na watu wa mkowa wa Upper Silesia nchini Poland, lakini pia kinazungumzwa katika nchi ya Ucheki na Ujerumani. Mnamo mwaka wa 2011, imetangazwa kuwa takriban 509,000[1] Kisilesia kuwa kama lugha yao fasaha.
Kisilesia kina husiana kwa karibu sana na lugha ya Kipolandi, na ndiyomaana kinafikiriwa na wanasiimu wengi kuwa kina lafudhi ya Kipolandi.
Herufi za Kisilesia
haririHakuna herufi moja tu ya Kisilesia. Wazungumzaji wa Kisilesia hutumia kuandika kilugha hiki kwa kufuata taratibu za uandikaji wa Kipolandi. Mnamo mwaka wa 2006 imegunduliwa herufi mpya za Kisilesia, ipo katika misingi ya Kisilesia tu (kuna misingi ipatayo 10). Kina tumika sana katika mtandao wa Internet, kama vile jinsi kinavyotumika katika Wikipedia ya Kisilesia.
Aa Bb Cc Ćć Čč Dd Ee Ff Gg Hh Ii Jj Kk Ll Mm Nn Ńń Oo Pp Rr Řř Ss Śś Šš Tt Uu Ůů Ww Yy Zz Źź Žž
Na baadhi ya herufi za ziada: Ch Dz Dź Dž.
Viungo vya nje
hariri- Habari kwa lugha ya Kisilesia
- Pů našymu – djalykt ślůnski kodyfikowůny Ilihifadhiwa 14 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- makala za OLAC kuhusu Kisilesia
- lugha ya Kisilesia katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/szl
- ↑ Narodowy Spis Powszechny Ludności i Mieszkań 2011. Raport z wyników - Central Statistical Office of Poland