Kiva ni kata mojawapo ya Wilaya ya Handeni vijijini katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, wakazi walikuwa 10,874 [1], wakati katika ile ya mwaka 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,972 waishio humo.

Kata hii inajumuisha jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Zavuza, Kwedibangala na Kweditiribe. Makao makuu ya kata ya Kiva yako kijiji cha Zavuza.

Katika vijiji hivyo kuna jumla ya shule za msingi nne pamoja na shule moja ya elimu ya sekondari iliyoanzishwa mwaka 2009.

Pamoja na yote hayo kata ya Kiva haina hospitali, ila wananchi wa kata hii wanategemea zahanati chache zilizopo. Wengine wanasema hospitali moja ipo katika kijiji cha Zavuza.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Handeni Vijijini - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Kabuku | Kabuku Ndani | Kang'ata | Kitumbi | Kiva | Komkonga | Kwachaga | Kwaluguru | Kwamatuku | Kwamgwe | Kwamsisi | Kwankonje | Kwasunga | Kwedizinga | Mazingara | Mgambo | Misima | Mkata | Ndolwa | Segera | Sindeni

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiva kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.