Kiwewe sugu cha ubongo cha Encephalopathy

ugonjwa wa neurodegenerative ulio na sababu ya jeraha la kichwa

Ugonjwa wa Kiwewe sugu cha ubongo cha Encephalopathy ni ugonjwa wa mfumo wa neva unaosababishwa na majeraha ya kichwa yanayorudiarudia.[1] Dalili zake huwa hazianzi hadi miaka kadhaa baada ya majeraha na zinaweza kujumuisha matatizo ya kitabia, matatizo ya hisia na matatizo ya kufikiri.[1][2] Ugonjwa huu mara nyingi huwa mbaya zaidi baada ya muda na unaweza kusababisha shida ya akili (dementia). [2] Haijulikani ikiwa hatari ya kujiua huwa inabadilishwa.[1]

Kiwewe sugu cha ubongo cha Encephalopathy
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuNeurolojia, Tiba ya Akili, Tiba ya Michezo
DaliliMatatizo ya tabia, Matatizo ya hisia, Matatizo ya kufikiri[1]
Miaka ya kawaida inapoanzaMiaka baada ya majeraha ya awali[2]
VisababishiMajeraha ya kichwa ya mara kwa mara[1]
Sababu za hatariMichezo ya inayohisisha kugusana, Jeshi, Unyanyasaji wa nyumbani, Kugongwa kichwa mara kwa mara[1]
Njia ya kuitambua hali hiiUchunguzi wa maiti[1]
Utambuzi tofautiUgonjwa wa Alzheimer, Ugonjwa wa Parkinson[3]
Matibabuhuduma za kupeana usaidizi[3]
Idadi ya utokeaji wakeHaijulikani[2]

Visa vingi vilivyorekodiwa vimetokea kwa wanariadha wanaohusika katika michezo ya mawasiliano kama vile ndondi, kandanda ya Marekani, mieleka ya kitaaluma, mpira wa magongo wa barafuni, raga na chama cha kandanda (soka).[1][4] Sababu zingine za hatari ni pamoja na kuwa jeshini, unyanyasaji wa nyumbani wa hapo awali na kupigwa kichwa mara kwa mara.[1] Kiasi kamili cha kiwewe kinachohitajika ili hali hii kutokea hakijulikani, na utambuzi wa uhakika unaweza kutokea tu wakati wa uchunguzi wa maiti.[1] Ugonjwa huu umeainishwa kama ugonjwa wa tau (tauopathy).[1]

Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa huu. [3] Viwango vya ugonjwa huu vimepatikana kuwa karibu 30% kati ya wale walio na historia ya majeraha mengi ya kichwa, [1] hata hivyo viwango vya idadi ya watu havijulikani.[2] Utafiti wa uharibifu wa ubongo kutokana na majeraha ya kichwa mara kwa mara ulianza katika miaka ya 1920, wakati huo hali hiyo ilijulikana kama dementia pugilistica au "punch drunk syndrome".[1][3] Imependekezwa kuwa sheria za baadhi ya michezo zibadilishwe kama njia ya kuuzuia.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 Asken, BM; Sullan, MJ; DeKosky, ST; Jaffee, MS; Bauer, RM (1 Oktoba 2017). "Research Gaps and Controversies in Chronic Traumatic Encephalopathy: A Review". JAMA Neurology. 74 (10): 1255–1262. doi:10.1001/jamaneurol.2017.2396. PMID 28975240.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Stein, TD; Alvarez, VE; McKee, AC (2014). "Chronic traumatic encephalopathy: a spectrum of neuropathological changes following repetitive brain trauma in athletes and military personnel". Alzheimer's Research & Therapy. 6 (1): 4. doi:10.1186/alzrt234. PMC 3979082. PMID 24423082.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Alzheimer's & Dementia". Alzheimer's Association. alz.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Maroon, Joseph C; Winkelman, Robert; Bost, Jeffrey; Amos, Austin C; Mathyssek, Christina; Miele, Vincent (2015). "Chronic Traumatic Encephalopathy in Contact Sports: A Systematic Review of All Reported Pathological Cases". PLOS One. 10 (2): e0117338. Bibcode:2015PLoSO..1017338M. doi:10.1371/journal.pone.0117338. PMC 4324991. PMID 25671598.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiwewe sugu cha ubongo cha Encephalopathy kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.