Mtakatifu Kizito (1872 - Namugongo (Uganda) 3 Juni 1886) ni mmojawapo wa Wafiadini wa Uganda, mdogo kuliko wote.

Alichomwa moto kwa ajili ya imani yake kwa Yesu Kristo akiwa na umri wa miaka 14 tu.

Pamoja na wenzake alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1964 huko Roma.

Sikukuu yake ni tarehe 3 Juni kila mwaka.

Ni msimamizi wa watoto na wa shule za msingi.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • J. FRANSE, W.F., Mashahidi 22 wa Uganda – tafsiri ya C. Kuhenga n.k. – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1981

Viungo vya njeEdit