Kobbie Boateng Mainoo (amezaliwa 19 Aprili 2005) ni mchezaji wa kandanda wa Uingereza ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza. Anajulikana kwa chenga, utulivu, na uwezo wa kiufundi anaokuwa nao pindi akiwa dimbani, anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji chipukizi bora zaidi duniani.[1][2]

Kobbie Mainoo akishangilia goli na wachezaji wenzake wa Manchester United

Mainoo ni mhitimu wa kikosi cha vijana wa Manchester United na alishinda tuzo ya Jimmy Murphy mchezaji bora chipukizi wa mwaka mnamo 2023. Alicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza katika mechi ya kombe la EFL Januari 2023. Mainoo aliichezea Uingereza kutoka ngazi ya vijana chini ya umri wa miaka 17, kabla ya kukipiga mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa mnamo Machi 2024.

Marejeo

hariri
  1. "The best young footballers in the world - ranked". 90min.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2024-07-17. Iliwekwa mnamo 2024-12-28.
  2. James Evans, Callum Bishop (2024-01-04). "The 20 best young players in the Premier League right now ranked in order". GiveMeSport (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-28.
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kobbie Mainoo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.